Apr 19, 2015

Mtunis Atoboa Haya Kuhusu Tasnia ya Filamu

Mtunis Atoboa Haya Kuhusu Tasnia ya Filamu
Staa wa Bongo Movies, Nice Mohammed ‘mtunis’ amesema kuwa tasnia ya uigizaji inahitaji umakini zaidi ili kujikosoa penye makosa. Alisema licha ya kwamba  filamu zinadaiwa  hazilipi hiyo  siyo sababu yakutayarisha zisizokuwa na ubora.
Alifafanua hata wakongwe wanapoibua chipukizi wanapaswa kuzingatia wenye vipaji zaidi ili tasnia huyo iendelee kufanya vizuri .
Alieleza kuwa hakuna kitu kibaya kama mtu anayekuamini akikudharau harudi nyuma, hivyo kwa kuwa makini kutayarisha filamu bora na hadithi tofauti ni kuzidi kujenga imani kwamashabiki na wadau wa filamu.
“Kujikosoa ndiyo dawa, hayo mengine tunatapatapa, filamu nzuri na zenye viwango zipo,kuna watu wanafanya kazi inaonekana, hivyo ni jukumu la kila mmoja kujipima, kama anaitendea haki tasnia na anataka  kuwepo kwa miaka 10 ijayokutokana na filamu anazo igiza au kutayarisha”-alisisitiza Mtunis.

na bongomovies.com