Tume ya uchaguzi nchini Sudan
inasema kuwa imeongeza mda wa kupiga kura ya urais na ubunge hadi siku
ya alhamisi huku ripoti za idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza
zikitolewa.
Kura hiyo imesusiwa na upinzani ambao unasema kuwa
idadi hiyo ya wapiga kura inaonyesha raia hawajali na kwamba kuna
uwezekano mkubwa kwamba rais Omar Al Bashir atatangazwa mshindi.Bwana Al Bashir amekuwa mamlakani tangu mwaka 1989.
Rais wa Sudan Omar Al Bashir
Shughuli ya upigaji kura ilitarajiwa kuchukua siku tatu na kukamilika leo.Mkuu wa tume ya uchaguzi alisema kuwa alitarajia idadi ya wapiga kura ijitokeze na kufikia asilimia 45.

