
Ofisa
polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Rashid Msuya akiwafundisha wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mapambano Sinza jijini Dar es Salaam jinsi ya kuvuka
barabara kwa kutumia alama za barabarani, ikiwa ni mwendelezo wa
kuadhimisha siku ya Afya na Usalama kazini Duniani. Hafla hiyo
iliandaliwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika shule hapo.

Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Msasani A na B ya jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza
Ofisa polisi wa Usalama Barabarani (CPL) Rashid Msuya alipofika shuleni
hapo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania(Hawapo
pichani) kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Usalama barabarani.
Mkuu
wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare
(kushoto) akiwafafanulia jambo baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi
Mapambano.
Koplo
Theresia Bayona akitoa elimu ya sheria za barabarani kwa wanafunzi wa
Shule ya Msingi Msasani A na B iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa darasa la pili Juma Rashid wa Shule ya Msingi Msasani A na B iliyopo jijini Dar es Salaam,akionesha ujumbe.
Gane
Maikara kushoto na Patricia Stephano ambao ni Wanafunzi wa Shule ya
Msingi Msasani A na B ya jijini Dar es Salaam,Wakifundishwa jinsi ya
kuvuka barabara na Koplo Theresia Bayona (katikati).
Wanafunzi
wenye ulemavu wa kusikia wa shule ya msingi Msasani wakimsikiliza kwa
makini mwalimu wao Selestina Msangi wakati akiwafafanulia jambo juu ya
elimu ya utumiaji wa alama za barabarani.
Mustafa
Hussein ambaye ni mwafunzi mwenye ulemavu wa kusikia katika shule ya
msingi Msasani jijini Dar es Salaam (mwenye tisheti ya rangi ya damu ya
mzee) akifafanuliwa jambo na Ofisa polisi wa Usalama Barabarani (CPL)
Rashid Msuya,kuhusiana na sheria za alama za barabarani.
Ni katika mwendelezo wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama Duniani
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano na Msasani A na B zote za
jijini Dar es Salaam leo wamenufaika na mafunzo ya Afya na Usalama
barabarani ikiwa ni mwendelezo wa kuadhimisha siku ya Afya na Usalama
mahala pa kazi duniani na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa
kushirikiana na jeshi la Polisi Kanda ya Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es
Salaam ambapo elimu hii pia itaendelea kutolewa katika shule za msingi
zingine jijini mapema wiki hii.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo yalionekana
kuwavutia wanafunzi wa shule hiyo ambao pia walishiriki katika mazoezi
ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayojitokeza kwa dharura.
Akiongea juu ya mafunzo Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama wa Vodacom
Tanzania Karen Lwakatare,amesema Vodacom ikiwa ni kampuni inayozingatia
usalama wa wafanyakazi wake na watanzania wote kwa ujumla imeamua kutoa
mafunzo ya usalama sehemu za kazi kwa wanafunzi ikiamini kuwa wao ndio
wafanyakazi wa baadaye ambao ndio tegemeo la kukua kwa uchumi wetu.
“Tumeona pia kuna umuhimu kwa wanafunzi hawa kujua alama mbali mbali
za barabarani pamoja na matumizi yake mbali na kuishia kuziona tu kwa
macho. Kama suala la usalama barabarani lazima lipewe kipaumbele kwani
kama tujuavyo jiji la Dar es Salaam lina changamoto nyingi ukizingatia
magari sasa yamekuwa mengi kitu na matumizi ya barabara yanachanganya
watu wengi na kusababisha kuwepo na ajali nyingi za barabarani”.Alisema.