
Mfalme
wa Masauti Christian Bella ameachia Track yake mpya Nashindwa Audio
pamoja na Video, Audio ya wimbo huo imefanywa chini ya Studio za
Combination sound chini ya Producer man Walter na Video imefanyika
Africa ya Kusini na director kutoka Bongo Adam Juma, Christian Bella
amesema kuwa lengo la kwenda South Africa ilikua ni kufata location tu
na pia amesema kuwa madirector wa Bongo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya
video nzuri kwa sasa isipokuwa hawana connection za TV kubwa za Africa
na Nje ya Africa tofauti na Madirector wa SA ambao wana connection kubwa
ya TV Kubwa hivyo wakikufanyia Video inafika Mbali zaidi.

Mbali
na hilo Bella anatarajia kufanya show kubwa siku ya tarehe 18/4 na
inategemea kufanyika pale escape one huku msanii Alice mwenye asili ya
Kiganda lakini anaishi Sweden anatarajiwa kuwepo siku hiyo, Alice
amefanya Track kama Mpita Njia na Juliana lakini pia amefanya Yabolingo
Track ambayo imefanya vizuri sana hapa Tanzania na Est Africa kwa
ujumla. Wasanii wengine watakao shiriki siku hiyo bado hawajajulikana
lakini bella amesema kuwa anatarajia kufanya na wasanii wa THT na
wengine ambao bado wako kwenye mazungumzo na haitokuwa band yeyote ya
dance.