
Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki ya hiyo jana jijini Dar es Salaam. Wengine
ni Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga
(wa pili kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George
Binde (kushoto) .

Meneja Mwandamizi utafiti
na Uchambuzi wa Biashara wa Benki ya Exim Tanzania, Joseph Mrawa (wa
pili kulia) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo jana jijini Dar
es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim
Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) Mkuu
wa kitengo cha rasilimali watu wa benki hiyo , Frederick Kanga (wa pili
kulia) na Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo, George Binde
(kushoto)

Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (katikati ) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya mapato ya mwaka 2014 ya benki hiyo jana jijini Dar
es Salaam. Wengine ni Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki ya Exim
Tanzania Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kutoka kulia) naMkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo,George Binde (kushoto)
BENKI
ya Exim Tanzania imepata ongezeko la faida (kabla ya kodi) kwa mwaka
2014 la asilimia 35 kufikia shilingi bilioni 24.1 kutoka shilingi
bilioni 17.9 kwa mwaka 2013. Benki imeendelea kuwa na mali za shilingi
tilioni 1 na kuweza kukuza pato la wenyehisa kwa asilimia 23 kufikia
shilingi bilioni 190 ikilinganishwa na shilingi bilioni 154
iliyorekodiwa mwaka Jana.
"Tunafuraha
kubwa kuitangaza kwenu mafanikio makubwa ya kifedha ya mwaka 2014
Desemba,” alisema Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Issa Hamisi, akizungumza
na waandishi jijini Dar es Salaam Jana.
Alisema
kuwa benki hiyo imefanikiwa kupata faida (baada kodi) kiasi cha sh
bilioni 57.3 kutoka sh billion 44.2 iliyopatikana mwaka 2013 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 30, ikilenga zaidi katika ongezeko la amana zenye
gharama nafuu.
Kwa
mujibu wa Bw. Hamisi, pia masuala ya ada, kamisheni na mapato ya fedha
za kigeni yaliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia shilingi bilioni 38
kutoka shilingi bilioni 30.4 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu kwa kiasi
kikubwa umechangiwa na kasi ya ukuaji katika shughuli ya za biashara za
fedha za kigeni, bidhaa za biashara ya fedha na ada kutoka kwenye
utoaji wa huduma mbadala.
Mali
za benki zimekuwa wakati ‘Gross NPA ratio’ ikishuka kutoka asilimia 9.60
kwa mwaka 2013 kufikia asilimia 6.83 mwishoni mwa mwaka uliyolipotiwa.
Benki
hiyo pia iliweka mkakati wa miaka mitatu mwanzo kabisa wa mwaka huo 2014
ambao ulilenga kujiongezea soko lake la amana sambamba na kufikia
nafasi ya uongozi katika malipo.
Bw.
Hamisi aliongeza kuwa benki imeweka mkakati wa kuzidi kujiimarisha na
kuimarisha watu wake, shughuli zake pamoja na teknolojia. Alisema benki
imeweza kufanyakazi na makampuni bora ya kimataifa katika utoaji ushauri
kwenye masuala yajulikanayo kama Enterprise-wide Risk Management, na
pia kuweza kurahisisha zaidi ufanyaji wa shughuli zake kwa mwaka huo.
Aidha
Bw Hamisi aliongeza kuwa benki imendelea jitihada za kupanua wigo wa
huduma zake kwa kuongeza idadi ya matawi mawili kwenye nchi tatu ambazo
inatoa huduma zake vikiwemo visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.
“Mafanikio
haya ni mwangaza tosha katika utendaji wetu wa sasa na siku zijazo….kwa
sasa Exim imejenga msingi imara kitu ambacho kinatuhakikishia mafanikio
zaidi kwa mwaka huu 2015,’’ aliongeza Bw Hamisi.
Benki
imeendelea kujidhatiti katika urejeshaji wa kile ikipatacho toka kwa
jamii. Katika mwaka huo benki ilijikita zaidi katika kusaidia taasisi za
elimu, hospitali na taasisi nyinginezo.
na michuzi media