Nyota
wa muziki Keisha ambae aliwahi kutamba na nyimbo kama
Usinicheke,Uvumilivu na Zawadi amefunguka na kusema kuwa kifo cha mdau
wa muziki nchini ambaye ni Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi
la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale 'kimemuumiza
kwani ndiye aliyekuwa msimamizi wa kazi za Keisha kabla hajatoka katika
kundi la Tip Top Connection na
kuanza maisha ya muziki akiwa kama Solo Artist,Keisha amesema Abdu Bonge alikuwa zaidi ya Boss kwake,maana aliweza kumjenga na kumtengeneza katika misingi mizuri ambayo Keisha anaamini ndiyo urithi mkubwa aliobakiwa kutoka kwa Abdu Bonge,ambae amefariki Jumamosi ghafla.
Keisha ameeleza kuwa Abdu Bonge alikuwa kama mzazi kwake maana aliweza kumfanyia mambo mengi na kuhakikisha anapata kila jambo ambalo alilihitaji kwa wakati
"Ni miaka kumi imepita tangu tukutane kwa mara ya kwanza ukawa boss. Kaka. Rafiki na hadi ukawa baba kwamaana ndiyo baba uliyekuwa karibu kwenye matatizo yangu yote nakumbuka ulipokuwa unanifuta machozi nilipokuwa nalia. Nakumbuka tulipo kuwa tukikesha studio tukiwa na mdogo wako Babu tale nakumbuka uliponifanyia birthday party kubwa nikiwa na miaka ishirini nakumbuka ulipokuwa unawafanya watu waone kila nilichokua nahitaji toka kwako nilipata."
"Nakumbuka siku niliyokuja kukuaga kwamba natoka Tip Top uliridhia na kunipa baraka zote kwakuwa uliamini nipo sahihi nakumbuka vingi sana hivyo ni vichache ila kubwa pale uliponihusia hata kama nafanya music nisisahau kujihifadhi na kumrudia mungu wangu kwakuwa duniani tunapita na mimi sasa ni mke wa mtu natakiwa nijheshimu." Aliongeza Keisha.
Mbali hilo Keisha anaonyesha wazi kuumizwa na msiba huo kwani anaamini huenda asipate mtu ambaye anaweza kumshauri kama alivyokuwa akifanya Abdu Bonge
"Umeondoka na umeniacha nikiwa sina mshauri tena ndomana wiki iliyopita nilipopita pale uliniita kwa sauti kubwa na nikashuka kwenye gari kumbe ulikuwa unaniaga boss wangu dah nilikupenda sana na ulilijua hilo ila mungu amekupenda zaid.Insha Allah tunakuombea dua siku zote ulale mahali pema peponi ameen kipenzi cha wengi abdu bonge ahsateni sana wote kwa kuja kumzika mpendwa wetu mungu awabariki.
Abdu Bonge alifariki siku ya Jumamosi usiku alipokuwa akiamulia ugomvi kati ya wapenzi wawili waliokuwa wakigombana,alipoamulia ugomvi alisukumwa na kuanguka chini na kupelekea kifo chake na siku ya Jumanne Abdu Bonge alizikwa kijijini kwao Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro.
chanzo:eatv.tv