HAIKUWA rahisi kugundua na kubaini vibwagizo vya Mkude Simba
vilivyoibuka ghafla kuteka jiji la Dar es Salaam pamoja na nchini nzima
mwasisi wa wazo hilo alikuwa ni Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ anasema kuwa
wazo hilo liliandaliwa kwa muda wa miaka miwili na kuja kuteka umma.
“Wazo la Mkude Simba nilikuwa nalo toka mwaka 2012 lakini nilipokuwa
najaribu kulitumia baadhi ya Redio zilishindwa kunielewa, lakini Efm
walinielewa na kutumia vibwagezo vyangu vya Mkude Simba,”anasema Kitale.
Kitale anasema kuwa baada ya kufanikiwa kujenga alama ya uhusika wa
mtumiaji wa madawa ya kulevya ‘Teja’ alikuwa akiumiza kichwa anaweza
kuibuka na kitu gani cha kibunifu na kuteka hadhira, katika kulinda kazi
zake anatarajia kufungua kampuni yake na kazi yake ya kwanza itakuwa
Harusi ya Teja.
