Wito huo ulitolewa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa droo ya 45 ya Promosheni ya Jaymillions ambayo imemuwezesha mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kitita cha shilingi Milioni 100/- ingawa alipopigiwa simu na maofisa wa kampuni hiyo mbele ya waandishi wa habari na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Mrisho Millao simu ya mteja huyo ikawa haipatikani.
“Tunaelewa zipo sababu zisizoweza kuzuilika ambazo zinaweza kusababisha simu ya mteja isiwe hewani lakini vilevile kuna baadhi ya wateja wana utamaduni wa kuzima simu ambao unaweza ukasababisha mteja akose mawasiliano ya muhimu kama mteja wetu huyu leo ambaye tulitaka kumpa taarifa ya kujishindia kitita chake kupitia promosheni yetu ya Jaymillions”.
Alisema kwa mjibu wa taratibu za Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa namba hiyo ya ushindi kutopatikana wataendelea kufanya jitihada za kumtafuta mshindi kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari na kuendelea kumpigia mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili kuona kama kuna wakati atakuwa hewani.
Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari mwaka huu ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi wawili wa milioni 100/-(akiwemo mshindi wa leo),washindi wanne wa Milioni 10/-na washindi 38 wa Milioni 1/-
Nkurlu pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions katika kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.