Mar 23, 2015

Video: Mcheza Mieleka wa Mexico afia ulingoni mbele ya maelfu ya watazamaji

  
Mcheza Mieleka maarufu wa Mexico Hijo del Perro Aguayo, amefariki dunia akiwa ulingoni mbele ya maelfu ya watazamaji weekend iliyopita.
Mwana mieleka huyo alikuwa akipambana na Rey Mysterio Ijumaa iliyopita. Alikimbizwa hospitali lakini madaktari walithibitisha kuwa amefariki dunia saa saba usiku March 22.
Hijo del Perro Aguayo (35) ni mtoto wa mchezaji mkongwe wa mchezo huo wa Mexico Pedro ‘Perro’ Aguayo.