Mrembo na mwigizaji wa filamu Shamsa Ford amewafungukia watu
wanaoeneza taarifa kuwa ameachana na mumewe, Dickson Matoke kwamba
hakuna kitu kama hicho.
Uvumi wa Shamsa kuachana na mumewe umechangiwa hasa na Shamsa
mwenyewe kutokan na “posts” anazoweka mtandaoni kwa siku za hivi
karibuni, kwani zimekuwa kiziongelea maswala ya mapenzi na hasa swala la
kutendwa katika mapenzi huku akiwasifia wanawake kwa moyo wao wa
kupenda na kuweka picha zaidi akiwa na mototo wake pekee na kusema hiyo
ndio furaha yake, tofauti na zamani ambapo alikuwa akiwepa picha akiwa
na mume wakepamoja na motto na kuandika maneno ya upendo.
Akizungumza na gazeti moja hivi juzi kati, Shamsa alisema kuwa
hajaachana na mumewe huyo na wote wanaosema hivyo watakuwa
wanamtaka.“Bado nipo na mume wangu tena kajaa tele, nashangaa hao
wanaosema kuwa tumeachana labda wanamtaka,” alisema Shamsa.
