Umoja wa mataifa unasema kuwa
vijana wa kiume waliotekwa juzi nchini Sudan Kusini huenda
walichukuliwia na kundi la wapiganaji lenye uhusiano na serikali.
Shirika
la watoto la umoja wa mataifa UNICEF linasema kuwa idadi ya watoto
waliotekwa na kundi la Shilluk walikuwa mamia na sio 89 jinsi
ilivyoripotiwa awali.Walioshuhudia walisema kuwa wengi wa watoto hao wamepelekwa kwenye kambi ya mafunzo kwenye jimbo la Upper Nile na watoto walio hadi chini ya miaka 12 walikuwa wakibeba bunduki.
BBC
