Mfanyakazi wa kampuni ya Endless Fame, Petitman ambaye mara zote
ameonekana kuwa karibu sana na bosi wake , Wema Sepetu amesema kamwe
hawezi kuacha kuwa karibu na Wema eti kwa sababu Wema na Diamond
wameachana, ukizingatia kuwa Pititman na
Diamond ni mtu na shemeji
yake. (Petitman amemuoa dada yake Diamond, Esma)
Kauli hiyo inaashiria kwamba Petitman yupo tayari kunyang'anywa mke
endapo uhusiano wake na Wema Sepetu hautaipendeza familia ya Diamond
kuliko kuvunja uhusiano na Wema Sepetu ..
Petitman aliyasema hayo redioni alipoulizwa kama kuvunjiaka kwa
mahusiano kati Wema na Diamond yana weza kutatiza ndoa yake na dada wa
Diamond.
Alisema "Mimi na Wema ni Damu Damu ...ila mambo ya mahusiano kila mtu na mambo yake hatuingiliana wala…”.
Pititman na Wema kwasasa wanaonekana kuwa karibu zaidi na masanii
Ommy Dimpoz ambapo wote wawili wameshiriki kwenye video ya wimbo mpya wa
msanii huyo unokwenda kwa jina la Wanjera.
Na BONGO MOVIES.COM
