Nyamiti kayora akiwa na vijana wa kikundi ch sanaa kutoka PAMOJA YOUTH wakiwa na furaha na kumuonesha nyamiti kuwa wao wamepokea ujumbe wake wa kuonesha upendo dhidi yao walifanya michezo mbali mbali ikiwemo sarakasai mpira na kuimba nyimbo nzuri sana.
Nyamiti kayora katikati ameketi akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa SAHARA MEDIA GROUP. Star Tv na RFA KISS FM wakifuhaia siku ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo mtangazaji wa Star tv huku burudani zikiendelea ndani ya ofisi na vile vile kazi zikiendelea kufanyika kwa ufanisi zaidi.
Nyamiti ameiambia blog hii kuwa kitendo cha yeye kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto walio katika mazingira magumu ni moja ya kuwatia moyo na kuwapa faraja kwani hata wao wanatakiwa kuthaminiwa na kutambuliwa katika jamii. amesema kuwa watoto wanatakiwa kupewa vipaumbele na kuwaonesha upendo na kuwafundisha baadhi ya mambo mazuri yenye maadili hata siku ikitokea wamepata fursa katika jamii basi waweze na wao kutambua uwepo wa wenzao waliopo ktika mazingira magumu nyamiti ameisisitiza kua watu wasiwe wanawatenga watoto hao bali pale waonapo kuna fursa ya kuwapa msaada basi waweze kujitolea na kuwasaidia ili na wao maisha yao yawe kama ya binadamu wa kawaida anayehitaji mahitaji muhimu kama vile Chakula mavazi na hata maladhi na hiyo pia itaongeza thawabu kwa Mungu.
watoto wa kikundi cha PAMOJA YOUTH kilichopo jijini mwanza






























