Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akiwahutubia washiriki wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni
lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika
Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana Jijini Dar es Salaam na kuhusisha
washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya
lugha ya kiswahili.
Rais
wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz akizungumza na
washiriki wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana katika
Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw.
Ali Akkiz wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni jana
katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu
katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel kushoto akifurahia maonyesho mbalimbali yaliyokua
yakionyeshwa na vijana wakati wa Tamasha la Kimatafa la Lugha na
Utamaduni jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kilimanjaro
Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz na wapili kulia ni Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.
Washiriki
kutoka nchi 19 wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea
katika Tamasha la Kimatafa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na
Kilimanjaro Dialogue Institute na kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu
Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
kutoka shule za Feza wakiburudisha wakati wa Tamasha la Kimatafa la
Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute na
kufanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana jijini Dar es Salaam na
kuhusisha washiriki kutoka nchi 19 wakiwa na lengo la kuhamasisha
matumizi ya lugha ya kiswahili.
…………………………….
Na Lorietha Laurence na May-Zuhura Simba -Maelezo
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
ameeleza kuwa lugha ina mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa
itakuzwa sambamba na maendelao ya teknolojia.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni na kufafanua kuwa tamasha hilo limeonyesha kukua kwa lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi yetu tangu kupatikana kwa uhuru.
Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni na kufafanua kuwa tamasha hilo limeonyesha kukua kwa lugha ya Kiswahili ambao ni utambulisho wa nchi yetu tangu kupatikana kwa uhuru.
“Mkusanyiko
wa leo umeanzisha safari ndefu ya kukuza lugha yetu ya Taifa toka ngazi
za chini hadi za kimataifa, hivyo Tanzania imefarijika kuwa mwenyeji wa
shughuli hii muhimu “alisema Mhe. Dkt. Mukangara.
Aliongeza kuwa kwa upande wa serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya kufundishia kuanzi shule ya Msingi hadi Elimu ya Juu.
Aliongeza kuwa kwa upande wa serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali ya kukiendeleza Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya kufundishia kuanzi shule ya Msingi hadi Elimu ya Juu.
Dkt. Mukangara ametoa wito kwa vijana kujifunza Kiswahili na kuitumia lugha hiyo kuweza kujipatia ajira kwa kutangaza utumiaji wa bidhaa za lugha na utamaduni ambazo zina thamani kubwa kiuchumi.
“Lugha ni sawa na kiwanda ikitumiwa vizuri italeta ajira kwa jamii husika na kutumika kama lugha ya kufundisha wageni mbalimbali wanaokuja nchini na hata nchi za nje kwa kuipa hadhi ya kuzungumzwa sehemu mbalimbali” alisema Mhe. Dkt. Mukangara
Kwa Upande wa muandaaji wa tamasha hilo ambaye ni Rais wa Asasi za Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Ali Akkiz amesema kuwa kupitia tamasha hilo wameweza kutangaza vivutio mbalimbali vya kiutamaduni vya jijini Dar es salaam na Zanzibar.
“Kwa kweli watoto wamefurahi kushiriki katika tamasha hili kwa kuweza kutembelea sehemu zenye vivutio vya utamaduni pamoja na historia najua wataondoka na taswira nzuri ya kutokuisahau nchi ya Tanzania” alisema Bw. Akkiz
Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni ni la kumi 13 kufanyika ambalo limeshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 12 hadi 18 kutoka katika nchi 19 na nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili kwa mara ya kwanza.