Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana
(kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa 'Mpe Riziki si
Matusi" kumlinda mwanamke dhidi ya ukatili katika masoko wakati
akiuzindua Dar es Salaam jana. Mradi huo unaendeshwa na Shirika la
Equality for Growth (EfG). Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Diwani wa Kata
ya Ilala, Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita na Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Ilala, Nora
Mzeru
.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (katikati), akitoa hutuba
fupi mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri Chana Pinda (kulia). Kushoto ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya
Ilala, Nora Mzeru.
Mkurugenzi
Mtendaji wa EfG, Jane Magigita (kushoto), akimkaribisha Naibu Waziri
Dk.Pindi Chana baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Mmoja wa wadau waliofadhili mradi huo akisalimia wageni waalikwa.
Wanawake wafanyabiashara kwenye masoko mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Dk.Pinda Chana.
Mgeni
rasmi Dk.Pindi Chana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
wanawake wafanyabiashara masokoni na wadau wengine baada ya kuzindua
mradi huo.
Baadhi ya maofisa wa EfG (wenye sare) na wadau wengine wakisakata rhumba kwenye hafla hiyo
Diwani
wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (kulia), akicheza ngoma ya kabila ya
Wahehe iliyokuwa ikipigwa na kikundi cha Sanaa cha Machozi kilichokuwa
kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.
Hapa ni burudani kwa kwenda mbele.