Mwigizaji na mwanamuziki kutoka Bongo Baby Madaha amefunguka kwa
kusema kuwa wakati ukifika wa kuzaa anahitaji kuzaa mtoto mmoja tu wa
kiume katika maisha yake, na hilo litafanyika baada ya kukamilisha
miradi yake ambayo ipo karibuni kukamilika.
“Nahitaji kuzaa mtoto mmoja tu wa kiume, ndio malengo yangu, so
nilichofanya kwa sasa ni kujipanga ili mwanagu asipate taabu, nimefungua
kampuni ya Advanced Entertainment Studio,”anasema Baby Madaha.
Baby anasema kuwa suala la kuzaa ni la kujipanga na kuamua utaishije
kwa ajili ya kumsaidia mtoto wako bila kumtegemea mwanaume kwani atazaa
mtoto kwa mapenzi yake hapendi ikitokea hivyo asisumbuke kwa malezi,
angependa mwanaye amlee mwenyewe.
