Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akiweka sahihi katika mashine ya kielektroniki
za
Biometric Voters Registration (BVR),wakati akijiandikisha katika daftari
la kudumu la wapiga kura juzi katika kituo cha shule ya msingi
Ludewa mjini ,wa pili kulia anayeshuhudia ni kamishina
wa tume ya Taifa ya uchaguzi
(NEC) Prof Amone Chaligha(picha na
Na MatukiodaimaBlog,
Ludewa
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema mchakato wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu
la Wapigakura ulioanza kwa awamu ya pili katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
umeanza vyema na sasa mashine hivyo za kielektroniki za
Biometric Voters Registration (BVR), zinafanya kazi vizuri hata kwa wale
wenye vidole vyenye sugu.
Kauli hiyo
imetolewa jana na kamishina
wa tume ya Taifa ya uchaguzi
(NEC) Prof Amone Chaligha wakati
akizungumza na wanahabari nje ya
kituo cha kuandikishia wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani Ludewa mara baada ya mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe na msimamizi wa zoezi
hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumaliza
zoezi la kujinadikisha .
Alisema kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali
zilikuwa zikisumbua kutosoma alama za
vidole kwa baadhi ya watu hasa wale
wenye sugu kwa sasa kasoro hizo
zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi
ili kufanya kazi kwa mazingira yoyote yale .
Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa
ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa
litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo
mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha wala
kuhofu mashine kutofanya kazi .
Alisema tokea zoezi hilo lianze
wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa
Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia
kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.
“ Ni kweli siku
mbili tatu kasoro za sugu
katika vidole lilikuwa ni
shida ila wataalam wa IT walilifanyia kazi na kwa sasa
hakuna kasoro kama hizo na kuwa amepata kuzungukia
vituo mbali mbali mjini Ludewa na
vijijini kasoro kama hiyo
haipo tena kwa sasa
hata wakulima wanajiandikisha bila shida.
“
Kuhusu kasi ndogo
ya uandikishaji alisema
imechangiwa na waandikishaji
wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi kila mwananchi anapaswa
kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4
na kuwa kwa siku moja mashine inauwezo wa kuandikisha kiwango
cha chini kabisa ni kati ya watu
50 -80.
Hata hivyo
alisema wanaofanya kazi hiyo
ya uandikishaji ni wale ambao wanataaluma ya IT na walifanyiwa mchujo na wale
walioshindwa waliachwa hivyo wamejipanga
kuna kazi hiyo inafanikiwa
vilivyo.
Awali wakazi wa
Ludewa mjini waliokutwa kituoni
hapo walielezea kero kubwa ya
kukaa kwa muda mrefu kituoni
hapo bila ya kujiandikisha kwa madai ya watoa huduma
hiyo kufanya kazi kwa kasi
ndogo zaidi alisema mmoja kati ya wakazi hao Bw Ernest Yohana
.
Alisema kwa upande
wake alifika kituoni hapo toka majira ya saa 4 asubuhi na kukaa kwenye foleni hadi saa 9 ;30 alasiri
alipofanikiwa kujiandikisha na kuwa
kwao wakulima wanapotezewa
muda mwingi .
Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo
Filikunjombe ambae alifika kujiandikisha
akizungumza mara baada ya
kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo
vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na
mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi
yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.
“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa
leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia
kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza
katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa
mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na
mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.
Hata
hivyo aliipongeza NEC kwa
kufanya kazi kwa ratiba na kuwataka
kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa
kuzingatia muda zaidi
ili kuwawezesha wananchi
kwenda katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Pia
alisema kuwa propaganda za
kuwa vidole vyenye
sugu mashine haisomi kuwa
hazina ukweli kwani yeye ni mbunge
mwenye sugu katika vidole pamoja na wananchi wake
ila hakuna aliyelalamika
kushindwa kujiandikisha kwa ajili ya tatizo la sugu .
Alisema kama mtanzania unapaswa
kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo
katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba
mwaka huu.
Filikunjombe aliyasema hayo katika
kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati
akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi
wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya
wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa siku saba kabla ya kwenda
mikoa mingine ya Katavi,Ruvuma,Lindi na Mtwara .zinafanya kazi vizuri hata kwa wale
wenye vidole vyenye sugu.
Kauli hiyo
imetolewa juzi na kamishina
wa tume ya Taifa ya uchaguzi
(NEC) Prof Amone Chaligha wakati
akizungumza na wanahabari nje ya
kituo cha kuandikishia wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani Ludewa mara baada ya mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe na msimamizi wa zoezi
hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumaliza
zoezi la kujinadikisha .
Alisema kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali
zilikuwa zikisumbua kutosoma alama za
vidole kwa baadhi ya watu hasa wale
wenye sugu kwa sasa kasoro hizo
zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi
ili kufanya kazi kwa mazingira yoyote yale .
Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa
ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa
litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo
mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha wala
kuhofu mashine kutofanya kazi .
Alisema tokea zoezi hilo lianze
wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa
Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia
kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.
“ Ni kweli siku
mbili tatu kasoro za sugu
katika vidole lilikuwa ni
shida ila wataalam wa IT walilifanyia kazi na kwa sasa
hakuna kasoro kama hizo na kuwa amepata kuzungukia
vituo mbali mbali mjini Ludewa na
vijijini kasoro kama hiyo
haipo tena kwa sasa
hata wakulima wanajiandikisha bila shida “
Kuhusu kasi ndogo
ya uandikishaji alisema
imechangiwa na waandikishaji
wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi kila mwananchi anapaswa
kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4
na kuwa kwa siku moja mashine inauwezo wa kuandikisha kiwango
cha chini kabisa ni kati ya watu
50 -80
Hata hivyo
alisema wanaofanya kazi hiyo
ya uandikishaji ni wale ambao wanataaluma ya IT na walifanyiwa mchujo na wale
walioshindwa waliachwa hivyo wamejipanga
kuna kazi hiyo inafanikiwa
vilivyo.
Awali wakazi wa
Ludewa mjini waliokutwa kituoni
hapo walielezea kero kubwa ya
kukaa kwa muda mrefu kituoni
hapo bila ya kujiandikisha kwa madai ya watoa huduma
hiyo kufanya kazi kwa kasi
ndogo zaidi alisema mmoja kati ya wakazi hao Bw Ernest Yohana
.
Alisema kwa upande
wake alifika kituoni hapo toka majira ya saa 4 asubuhi na kukaa kwenye foleni hadi saa 9 ;30 alasiri
alipofanikiwa kujiandikisha na kuwa
kwao wakulima wanapotezewa
muda mwingi .
Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo
Filikunjombe ambae alifika kujiandikisha
akizungumza mara baada ya
kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo
vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na
mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi
yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.
“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa
leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia
kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza
katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa
mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na
mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.
Hata
hivyo aliipongeza NEC kwa
kufanya kazi kwa ratiba na kuwataka
kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa
kuzingatia muda zaidi
ili kuwawezesha wananchi
kwenda katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Pia
alisema kuwa propaganda za
kuwa vidole vyenye
sugu mashine haisomi kuwa
hazina ukweli kwani yeye ni mbunge
mwenye sugu katika vidole pamoja na wananchi wake
ila hakuna aliyelalamika
kushindwa kujiandikisha kwa ajili ya tatizo la sugu .
Alisema kama mtanzania unapaswa
kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo
katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba
mwaka huu.
Filikunjombe aliyasema hayo katika
kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati
akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi
wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya
wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa siku saba kabla ya kwenda
mikoa mingine ya Katavi,Ruvuma,Lindi na Mtwara .
Mwisho
|