Mkutano huo wa siku mbili utaambatana na mdahalo baina ya viongozi hao na wadau mbalimbali katika sekta za biashara na maendeleo. Mjadala wa viongozi hao utajikita katika umuhimu wa Ukanda wa Kati ambao ni kiungo muhimu katika ukuaji uchumi wa nchi hizo kwa kuwa husaidia katika uingizaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali kupitia Tanzania kwa njia za maji, reli na barabara. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao watafanya uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Uganda, Rwanda na DRC.
CHANZO: IRAN SWAHILI REDIO