
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokelewa na Mkuu mpya wa Wilaya ya
Hai,Mh.Anthony Mtaka,mara baada ya kuwasili na kupokelewa wilaya ya Hai
tayari kwa kuanza ziara ya wilayani humo.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuchimba msingi katika shule ya
msingi Modio-Masama Mashariki,Kinana alikagua na kujionea ujenzi mpya wa
shule hiyo msingi Modio iliyopata janga la tetemeko na kubomoka.

katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipita kwenye moja ya daraja maarufu sana
wilayani Hai,Dara la MNEPO lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji
cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika ukiendelea

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa daraja jipya la MNEPO
ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika,lililopo katika kitongoji
cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani
Hai,mara baada ya
kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana
ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi.

Baadhi
ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani
Hai,wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa staili ya aina
yake,alipokuwa akiondoka kijijini hapo mara baada ya kuzungumza nao
kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana
ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi. SOMA HAPA KUHUSIANA NA MGOGORO HUO

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kukagua chumba kipya cha
mionzi,pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Leonidas Gama.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifanya majaribio ya uchunguzi
juu ya mkono wake kupitia mashine mpya mionzi,iliyowekwa katika chumba
hicho cha mionzi.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa
hospitali ya wilaya ya Hai,mara baada ya kukagua chumba kipya cha Mionzi
(X-Ray).

Baadhi ya Wakazi wa mji wa Bomang'ombe wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa Snow View mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Bomang'ombe jioni ya leo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika uwanja wa Snow View wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.

Wananchi
wa Bomang'ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman
Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa
hospitali ya wilaya ya Hai,kabla ya kukagua chumba kipya cha Mionzi
(X-Ray).
habari kwa hisani ya JIACHIE BLOG