Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma
akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni kwa redio ya Jembe FM
ya jijini Mwanza kwenye ofisi za makao makuu ya TCRA jijini Dar es
Salaam.
Alisema
si radio tu ambayo ina nguvu ndiyo inayoweza kuhimili ushindani lakini
pia ufuataji wa kanuni na maadili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba
wameanzisha radio hiyo kwa lengo la zaidi ya kuburudisha na kuelimisha
bali kusaidia vijana kushika hatamu na kujitengenezea uwezo wa ajira.
Alisema
kwamba ili kuhakikisha kwamba wanafanyakazi kitaaluma wameajiri watu
ambao wamesomea kazi husika ili kuhakikisha kwamba hawaendi kinyume na
leseni yao.
Alisema
kwamba wanaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kujaza mapengo ambayo yapo
katika urushaji wa matangazo kwa sasa ili kuhudumia mji wa Mwanza ambao
unakua kwa kasi kwa sasa.
Mkurugenzi
wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi
(kushoto) akisisitiza jambo kwa uongozi wa JEMBE FM wakati wa hafla ya
kukabidhi leseni kwa uongozi huo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam
makao makuu ya ofisi za TCRA.
Alisema vipindi vyao vimezingatia haja ya jamii katika uchumi, elimu na afya. Aidha
amesema kwamba wanategemea kuwa na vipindi vizuri zaidi hasa kutokana
na na uzoefu waliokuwa nao hasa wa uandaaji wa njia ya panda. Jembe FM inamilikiwa na Jembe Media Limited.
Mkurugenzi
Mkuu wa Jembe FM Dk Sebastian Ndege (wa kwanza kushoto) na uongozi wa
juu kabisa wa Jembe Media Limited wakimsikiliza kwa makini kabisa
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya
kukabidhiwa leseni rasmi ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya
jijini Mwanza.
Baadhi ya wawakilishi wa kampuni ya Ndege Insurance inayomilikiwa na Dk. Sebastian Ndege waliojumuika kwenye hafla hiyo fupi.
Maofisa mbalimbali kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma
(kulia) akimkabidhi rasmi leseni ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE
FM ya jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege
(katikati) katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ofisi za TCRA
jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano
Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege akitoa neno la shukrani ambapo pia
maeahidi kuwa atafuata masharti na kanuni zote zilizowekwa na mamlaka
hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (wa
pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa juu kabisa wa
Jembe Media Limited. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Jembe Media Ltd.
Justine Ndege, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya Jembe Media Ltd, Renata Ndege.
Mkurugenzi
Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege na Mwanasheria wa Jembe Media Ltd.
Justine Ndege wakionyesha leseni hiyo iliyoambatanishwa na miongozi ya
Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
waliohudhuria hafla hiyo.
Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma
ametaka matumizi sahihi ya masafa ya radio yanayatumiwa kurusha vipindi
vya radio kwa ajili ya maendeleo ya umma.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akikabidhi leseni kwa radio Jembe FM.
Alisema matumizi yasiyo sahihi yatasababisha mamlaka hiyo kunyang’anya leseni walioitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Alisema
pamoja na haja ya kushiriki katika ushindani, kituo hicho kipya
kinatakiwa kufuata masharti ya utangazaji ambayo yamo katika leseni
waliyoiomba.
Alisema
radio hiyo ya Mwanza inaongeza ushindani katika eneo hilo katika jumla
ya radio FM 12 zinazosikika mjini humo, radio za kitaifa saba, za
kikanda 11 na radio ya jamii 1.
Aliwataka kuwa waangalifu na kufuata kanuni za kitaalamua kufanyakazi wanasotahili za kuelimisha na kuburudisha.