
Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mhe. Dkt. Titus Kamani akitembelea
mabanda ya maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayofanyika katika Jiji la
Paris nchini Ufaransa,na kujionea aina ya mifugo inayoshindanishwa. Hapa
anaangalia ng'ombe wa nyama aina ya Charolaise.

Mhe. Dkt. Kamani akiangalia kondoo wa sufi waliopo kwenye mabanda ya maonesho.

Umati
wa watu kutoka mataifa mbalimbali duniani waliohudhuria maonesho hayo.
Takriban watu milioni moja wametembelea maonesho hayo kwa mwaka huu 2015
ambayo hufanyika kwa muda wa siku tisa.

Mhe.
Dkt. Kamani pamoja na ujumbe wa watanzania wakisikiliza kwa makini
maelezo ya maendeleo ya sekta ya mifugo nchini Ufaransa na mfumo wa
uendeshaji wa maonesho ya kimataifa ya kilimo kabla ya kupata fursa ya
kutembelea mabanda mbalimbali.