BASI LAUA ZAIDI YA ABIRIA 40 BAADA YA KUANGUKIWA NA KONTENA IRINGA
ABIRIA zaidi ya
40 wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi la Majinja Express ambalo
lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kufunikwa na kontena
maeneo ya Changalawe, Mafinga mkoani Iringa muda huu.
Kwa mujibu wa
mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba dereva wa basi alikuwa akijaribu
kulipita lori ndipo walipodondokewa na kontena hilo.
Inadaiwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria 65 na abiria nane tu ndiyo walionusurika katika ajali hiyo mbaya.