Bango
la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma
FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na
Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry
Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha
wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu
zete Albino. .jpg)
Wachezaji
wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa
wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"
Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
Marafiki
wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni
mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine
.jpg) |
| Rafiki
wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM
Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni
maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo |
Na Henry Mdimu
Tangu
asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi
ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii
nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la
mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo
amekatwa mikono yake.
Wanasema
nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea.
Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka. Kwanza nalaani kitendo
hicho cha kikatili na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho
Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi
hivi.
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi?
Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu.
Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa?
#IMETOSHA