Feb 25, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE AKABIDHIWA RIPOTI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI KWA MAKAMPUNI YA UZIDUAJI NCHINI

 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Ngosi Mwihava (kulia) akimkaribisha  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) ili aweze kuzungumza na timu  ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya  kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya  Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii na Uwezeshaji  kwa  makampuni ya  uziduaji  yaani  madini na gesi. Timu  hiyo iliendesha zoezi hilo mapema Septemba, mwaka jana.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene akielezea umuhimu wa kuhamasisha makampuni mengi zaidi kujitokeza katika  kuwania   tuzo ya  Rais  katika utoaji  wa huduma kwa jamii na  uwezeshaji  kwa makampuni ya  gesi, mafuta na madini  ili  wananchi wafaidike zaidi na mchango katika sekta za nishati, madini na gesi.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (aliyekaa mbele) akizungumza na timu  ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya  kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya  Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii  na Uwezeshaji kwa  makampuni ya  uziduaji  yaani  madini na gesi. 
 
na JIACHIE BLOG