Feb 19, 2015

WAZIRI MEMBE AMUAGA RASMI BALOZI WA SAUDI ARABIA ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa ajili ya kumuaga   Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Mhe. Hani Abdullah Mominah  ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro tarehe 18 Februari, 2015.

Balozi Hani naye akitoa hotuba mbele ya wageni waalikwa.
Mhe. Waziri Membe akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora Balozi Hani
Picha ya pamoja .