Feb 26, 2015

TUZO KWA WASANII BORA WA ZANZIBAR KUFANYIKA KESHO

Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib, akimkabidhi Tuzo msanii, Rukia Ramadhan.
Kampuni ya Zanzibar Media Corporation ambayo ni wamiliki wa Zenji Fm Radio na gazeti la Nipe
Habari, kesho Ijumaa tarehe 27 February  wanatarajia kutoa tuzo kwa wasanii bora wa Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili Mratibu wa tuzo hizo Nd Said Khamis amesema jumla ya washiriki 76 wameshindania katika vipengele 20, na washindi wa vipengele hivyo wanatarajiwa kupewa tuzo na fedha taslim.
Aidha Said ameongeza kuwa tuzo hizo ambazo ni za 8 kufanyika mara hii zimeonesha kuwa kuna mwamko kwa wasanii wa Zanzibar kwa kuweza kutengeneza kazi nzuri na zenye ushindani katika tasnia ya musiki wa Zanzibar.
Sherehe hizi ambazo zitafanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Ikulu Dk Mwinyi Haji Makame.
+255 777 468189