“Wadau na wasanii wote mnaotaka kuigiza msidanganyike na account hii ya Facebook SIYO YANGU NI FAKE.
Maana napata tabu sana Ofisini kwangu watu wanakuja kudai Hela
wakisema kuwa Eti Mimi nimetangaza usahili kupitia kwenye account hiyo
hapo juu fake Kuwa nahitaji wasanii ni uongo mtupu mnaibiwa pesa zenu na
namba anayotumia kuwaibia Watu Hela ni hiii hapa 0779 946440.
Msidanganywe ni matapeli hao Mimi Sijatangaza Chochote kwenye Facebook. Im done hope That You Have All understood Me”.
Muigizaji Vicent Kigosi ‘Ray’ aliandika hayo mtandaoni mara baada ya
kubandika picha hiyo hapo juu ikionyesha account hiyo feki ilivyotoa
tangazo hilo.
Jamani tuweni makini na matapeli kwenye mitandao ya kijamii.
