Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe
"Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama
ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja
Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.
Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya
Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa
Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba
yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha
Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema,
"Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na
Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati
Utakapofika, Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu
Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."Zaidi
nawatakia Watanzania Kila la Kheri Katika harakati hizi".
Kila la kheri Ngwendulile kwani wao waweze wana nini na wewe ushindwe una nini? heno heno
BONGO MOVIES
