Jan 15, 2015

Rais Kikwete awasili maputo usiku kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa Msumbiji Mhe.Filipe

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Maputo usiku huu kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi kesho mjini Maputo. Mhe. Nyusi anachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Rais Armando Emilio Jacinto  Guebuza anayemaliza muda wake.