
.jpg)
Pia wanamuziki FFU-Ughaibuni kukosa Usingizi.
Imebainika
kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band
aka FFU-ughaibuni almaarufu viumbe wa ajabu Anunnaki Alien,inayoongoza
na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja,bendi hiyo
imejukuta ipo katika hali ya kukosa usingizi tena baada ya kutakiwa
kutumbuiza maomyesho zaidi katika msimu ujao wa joto.


watayarishaji wa
maonyesho makubwa ya nje barani ulaya wanashinikizwa na washabiki wao
lazima waipandishe jukwaani Ngoma Africa Band kutokana na mdundo wao
Bongo dansi,maporota hao baada kuweka roho juu na washabiki wao nao
wamedhamiria kuwapambanisha washabiki hao na bendi maarufu Ngoma Africa
band yenye makao yake nchini ujerumani.
Habari za uhakika zimetonya kuwa
bendi hiyo imekubali kuenda kutumbuiza katika nchi za Latvia na Austria
na maonyesho mengine katika msimu wa joto. habari zimetonya kuwa hali
hiyo tabia za washabiki kushinikiza katika maonyesho inaifanya bendi ya
Ngoma Africa band kuwa katika mzunguko wa maonyesho makubwa na
wanamuziki kukosa muda wa kupumzika.Lakini inasemekana kamanda Ras
Makunja na kikosi chake wanauwezo wa aina yake wa kuwamudu washabiki wao
waliodata akili na jinamizi la muziki wa dansi wa bongo kule barani
ulaya.ffu-ughaibuni pia wanasikika online at www.ngoma-africa.com.