Jan 20, 2015

Mirallas alipumzishwa sababu ya maumivu

Kocha wa Everton Roberto Martinez amesema sababu ya kumpumzisha mchezaji Kevin Mirallas ni majeruha aliyoyapata na sio kukosa mkwaju wa penati.
Mirallas alipumzishwa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Bryan Oviedo
"Kevin alipata matatizo ya misuli na tulimtoa kwa kuchukua tahadhari sio sababu ya kukosa mkwaju wa penati’’Alisema Martinez.

Bossi huyo ameeleza hakuna tatizo kati ya Leighton Baines na Kevin Mirallas kwa kawaida Baines ndio huwa anajukumu la kupiga mipira ya penati.
Kwa upande mwingine kocha Gary Brabin toka klabu ya Southport amejiunga na Everton na atahusika na kikosi cha chini ya miaka 21.