Mfalme wa Jordan na Rais wa
Palestinian Mahmoud Abbas ni baadhi ya viongozi kutoka Mashariki ya kati
walioshiriki katika maandamano yaliyofanyika mjini Paris Ufaransa
kulaani shambulio la kigaidi lililofanyika mjini Paris.
Morocco
haijawasilisha uwakilishi wa salam za rambi rambi kutokana na msimamo
wake tofauti na mwenendo wa Gazeti la Charlie Hebdo kutokana na vibonzo
ambavyo vimekuwa vikichorwa hasa vile vinavyolenga masuala ya kidini.Rais Hollande aliungana pia na Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu,katika Sinagogi la Grand kuomboleza kwaajili ya waathirika wane wa shambulizi la kigaidi katika Supermarket .
Netanyahu alimshukuru mmiliki wa Supermarket iliyoshambuliwa Lassana Bathily kwa jitihada zake katika kuwaokoa mateka waliokuwa ndani ya jingo hilo.

