Gazeti la kila wiki la vibonzo la
Charlie Hebdo la ufaransa toleo la kesho jumatano litarajiwa kuchapisha
kibonzo cha Mtume Mohamed katika ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa
cha habari "Yote yameshasamehewa"
Walioona kibonzo hicho wanasema
Mtume Mohammad ataonekana akishikilia bango lililoandikwa "Je suis
Charlie" maneno yenye tafsiri "mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha
mshikamano, baada ya shambulizi katika ofisi za gazeti hilo jumatano
wiki iliyopita ambapo wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo
waliuawa.Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho tayari zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala sitini elfu kwa wiki
