Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI mbali mbali zinazotoa huduma kwa jamii zinatarajiwa kutambuliwa na kutolewa tathimini ya uwajibikaji wake machi mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa
Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera alisema lengo ni kurudisha sehemu ya
biashara kwa jamii kama sehemu ya shukrani.
Alisema pia italeta faida nyingine ikiwa ni pamoja na kuleta
mahusiano mazuri na kampuni nyingine ambapo matoko yatakayotoka yataleta
hamasa kwa kampuni nyingine kurudisha sehemu yao ya biashara katika
jamii.
Hyera alisema tafiti zinaonesha kuwa kampuni za nje ndo zinahusika
zaidi katika jamii hususani katika masuala ya elimu, mindombinu, maji na
huduma nyingine za kijamii.
"Tayari kunataasisi nyingine zimeshafanya marejesho hayo na
nyingine hazijaleta hivyo nyingine zijitokeze kuonesha nia ya kushiriki
ili ziweze kunufaisha jamii," alisema.
Aliongeza kuwa mchakato huo pia unalenga kutathimini kwa
kulinganisha takwimu za mirejesho ambayo inafanywa na taasisi
kuthaminisha na kung'amua kuhusu manufaa hayo na gharama zake.
Alisema madhumuni makubwa ya tathmini hiyo yanajumuisha kuona jinsi
gani taasisi mbalimbali zinazojitoa kwaajili ya kusaidia jamii,
kutambua na kuthamini wanaofanya vizuri, jinsi taasisi hizo
zinavyochangia kufanya maisha ya wanajamii kuwa bora kwa kuzingatia
idadi ya misaada ambayo inatolewa na thamani zake.
Naye Katibu wa Kamati ya Tathmini Ernest Mamwaja alisema kuna watu
wananufaika lakini hawajui wamesaidiwa na nani hivyo watajua, pia
wanaotoa msaada wanaweza kuleta nguvu katika maeneo ambayo manufaa yake
ni makubwa.
Alisema tafiti ambazo zimeonesha kuwa kampuni ambazo zinarejesha
kwa jamii zinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na soko kupanda, hivyo
lengo si kuangalia nani mshindi au nani amefanyanini ali ni kwaajili ya
manufaa ya watanzania.