![]() |
| Huku wakizidi kuongezewa maarifa na manufaa ya semina husika, tayari wavuvi zaidi ya 2000 wameshajiunga na PPF. |
![]() |
| Pia wanasemina hao walipata fursa ya kuuliza maswali pamoja na kufanya majadiliano ikiwa ni sehemu ya kupima uelewa. |
![]() |
| PPF imeweka mikakati ya kuwafikia zaidi ya wavuvi 4000 katika wilaya ya Ukerewe. Aidha, PPF mapema mwakani ipo katika mkakati wa kufanya utafiti kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kukopesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali vilivyopo katika sekta zisizo rasmi. |
![]() |
| "Ndugu Meneja wa Kanda, napenda kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF ambao unatekeleza mojawapo ya sera zake ya kuhakikisha sekta isiyo rasmi inafikiwa kama ilivyo kwa sekta nyingine za uchumi hapa nchini. Hii itaongeza pato la Taifa hivyo kuzidi kuboresha maendeleo ya Watanzania kwa ujumla na kupunguza umaskini. Napenda kuwaambia kuwa kwa kuandaa semina hii muhimu katika eneo ambalo mimi mwenyewe nalisimamia imenipa faraja sana kwa kuona jinsi Mfuko huu wa PPF unavyowajali sekta zote za uchumu wa nchi. Hongereni sana." |
![]() |
| Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda ya Ziwa Ndugu Meshack Bandawe (pichani aliyesimama) alisifia Mahudhurio ya semina hiyo akisema kuwa yanadhihirisha kuwa kuna mwamko wa jamii ya watanzania kuhusiana na masuala ya hifadhi ya jamii unaendelea kukua na kuimarika. |
![]() |
| Wanasemina wakichukuwa data muhimu. |
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Mary Onesmo Tesha akitoa neno la shukurani pamoja na kukazia umuhimu wa mafunzo yanayotolewa kwa wananchi na vikundi kuhusu mifuko ya pensheni. |

IFUATAYO NI SEHEMU YA MWISHO YA HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT TITUS KAMANI (MB):-
Ndugu
Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, nitoe rai kwenu kuipa
nafasi semina hii muhimu ili muweze kuangalia wapi panahitaji kuboreshwa kwani hii
itawasaidia kupiga hatua katika uvuvi wenu. Kwani kwa taarifa nilizonazo zoezi
hili la kujiunga na PPF limefanikiwa sana ila changamoto kubwa ikiwa ni
uwasilishaji wa michango yenu PPF.
Napenda
kuwahamasisha kuwasilisha michango kwa wakati katika Mfuko wa PPF kwani ni
Mfuko mkongwe ambao vile vile umezidi kuboresha mifumo ya Tehama kwani sasa
kupitia simu ya mkononi unaweza kuwasilisha mchango wako kupitia M-pesa,Tigo
Pesa na Airtel money. Kwenu nyie kutokana na asili ya kazi yenu ya uvuvi njia hizi
ni muafaka zaidi katika kuwasilisha michango yenu kwa wakati.
Ndugu
Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, kwa kuwa nimeambiwa kuwa
hapa tulipo kuna viongozi wa wavuvi wasiopungua 50, hii inaashiria jinsi
mlivyolipa uzito suala hili la kujua manufaa yaliyomo ndani ya Mfuko wa PPF na
hatimaye muweze kujiunga. Sasa napenda niseme hivi, nyinyi viongozi mliofika
hapa mchukue jukumu la kusimamia zoezi hili katika maeneo yenu ya kazi ili
wavuvi wengi waweze kukwamua maisha yao kutoka uvuvi duni kwenda uvuvi wa
kisasa. Hivyo basi mnapaswa kuangalia kwa makini mambo yafuatayo:-
·
Kila kiongozi awe na orodha ya wavuvi
walioko katika kituo chake ambao tayari wamesajiliwa
·
Kila kiongozi lazima afahamu kilammoja
anachangia kiwango gani aidha kwa wiki au kwa mwezi na kuweka kumbu kumbu kwa
ajili ya mrejesho
·
Kila kiongozi awe na namba za simu za wavuvi
walioko katika kituo chake
·
Kila kiongozi ajiridhishe kila mvuvi
aliyejisajili awe na kitambulisho cha uanachama cha PPF
·
Kila kiongozi kuhakikisha anafahamu wavuvi
wote wasiojisajili na PPF au Mfuko wowote
·
Viongozi wote wachukue jukumu la kuhamasisha
wavuvi wote walioko katika vituo vyao wajiunge na kuchangia katika Mifuko ya
hifadhi ya jamii kama Mfuko wa Pensheni wa PPF
·
Vile
vile nitoe agizo kwa viongozi wote na
wawakilishi wa wavuvi wafanye kazi kwa karibu na ofisi ya PPF kanda ya
Ziwa kwa ajili ya ufanisi na manufaa ya wavuvi kwa ujumla
Ndugu
Meneja wa Kanda, baada ya kusema hayo, sasa naomba
niwakabidhi jukumu hili la kutoa semina kwa viongozi hawa wa wavuvi ili
mkawasajili wavuvi waweze kufaidika PPF ili kuboresha maisha yenu na ustawi wa
jamii. HABARI KAMILI KWA HISANI YA GSENGO BLOG/WAMBURABABU BLOG







