WaziriwaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wadau wa michezo ya Ngumina na Karate wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose.
Ulingo wa kisasa kwa ajili ya Mchezo wa Ngumi uliotolewa kama msaada na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL na kupokelewa naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akijaribu baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi (Gloves) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose na katikati yao mwenye suruali nyekundu ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Bw.Lukelo Willilo.