Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela
ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema
linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya
sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya
maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida
wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali
ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia
iliyopo Tengeru mjini Arusha. Alisema shirika lake limejikita zaidi
kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na
hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.
“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa
viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha
utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema
Naibu Mkurugenzi huyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida mara baada ya
kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi hiyo kushiriki mahafali hayo.
Akizungumza
mbele ya wahitimu wa Taasisi hiyo na Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba
sayansi na teknolojia vina nafasi ya pekee katika jamii na hivyo
shirika kama UNESCO inachofanya ni kusaidia kuwapo kwa elimu
hiyo.Alisema sayansi na teknolojia ni msingi wa maendeleo kwani kupitia
kuboreka kwa vitu hivyo viwili serikali nyingi zitaweza kukabiliana na
umaskini uliokithiri na kupeleka watu wake katika maendeleo na ustawi.
Kiongozi
huyo wa Unesco pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha kuwepo
kwa Taasisi hiyo ambayo ilibuniwa katika mkutano wa aliyekuwa Rais wa
Benki ya Dunia, James Wolfensohn, na Rais Nelson Mandela wa Afrika
Kusini mwaka 2001.Ubunifu huo ulifanyiwa kazi na viongozi wa nchi za
Afrika Januari 2005 katika mkutano wao wa Abuja ambapo walikubaliana
kuanzisha vyuo vinne vya sayansi na teknolojia kwa jina la Nelson
Mandela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu,
Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida
wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson
Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
Tengeru, mjini Arusha.
Alisema
sayansi inashikilia majibu ya maswali ya maendeleo ya Bara la Afrika
katika kukabili umaskini na kuwa na maendeleo endelevu katika sekta zote
na jamii. Naye Rais Kikwete akihutubia mkusanyiko huo aliwapongeza
viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuendeleza umaalumu wake.
“Taasisi
hii ni sehemu ya mtandao wa vyuo vya Nelson Mandela vya Sayansi na
Teknolojia katika Bara la Afrika. Chuo hiki cha Arusha ni mahsusi kwa
ajili ya kanda ya Afrika Mashariki. Ndiyo maana Hati Idhini (University
Charter) niliyokipa Chuo hiki inaeleza bayana kuwa Chuo hiki kinapaswa
kuwa chenye hadhi maalum (special status). Hadhi hii yapaswa pia
ionekane katika ubora wa elimu inayotolewa hapa. “ alisema Rais Kikwete.
Alisema ubora wake ni matokeo ya ubora wa wahadhiri wake, programu zake na miundombinu yake.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO), Getachew Engida akitoa kauli ya shirika lake kwenye
mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na
Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya
Afrika ya Nelson Mandela na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa juu wa
chuo hicho.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakifurahi
jambo wakati Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (hayupo pichani)
alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya
Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mwishoni mwa wiki
Tengeru jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Nelson
Madela, Sayansi na Teknolojia wakitoa burudani kwenye mahafali ya pili
ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati)
pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa
taasisi hiyo.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya
Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni
mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO
Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Rais
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa
(UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa
shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Pichani
juu na chini ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na
Teknolojia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Gharib Bilal akiwatunuku wahitimu mbalimbali wa shahada za juu za
uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi
wakati wa mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa
juma, Tengeru jijini Arusha.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria mahafali hayo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya maprofesa wa taasisi hiyo.
Pichani
juu na chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mahafali hayo.