Ujumbe wa Watalaamu wa masuala wa ICT, Ulinzi na Ujenzi kutoka Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) uko kwenye ziara ya mafunzo ( Study tour )
katika Mamlaka ya Bandari Ghana (GPHA) ili kubadilishana utaalamu wa
namna ya kuongeza ufanisi wa utekelezaji na kuimarisha Ulinzi wa
Bandari, ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa
ICT - TPA .
Kwa sasa TPA inatekeleza miradi kadhaa ya kuongeza ufanisi kwa kutumia ICT, kuboresha Ulinzi kwa kufunga Mitambo ya kielektroniki na kuongeza vifaa na maeneo ya operations ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari za Dar, Mtwara na Ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo na Mwambani Tanga.
Ujumbe wa TPA ukiongozwa na Ndg. Magesa wakiwa kwenye mazungumzo na
wenyeji wao kutoka Mamlaka ya Bandari ya Ghana kufanya majumuisho ya
ziara .
Watalaamu wa TPA wakiwa kwenye chumba Chenye vifaa vya kielektroniki Cha
kuangalia matukio ya kuilinzi na ki usalama katika Bandari ya Tema
Watalaamu wa TPA toka idara za Ujenzi, TEHAMA na Ulinzi wakiangalia
Ujenzi wa Magati manne ya kisasa katika Bandari ya Tema , Ghana
Watalaamu wa TPA wakiangalia lango la kuingia bandarini ambazo lina
vifaa maalumu vya ki electronic vya kutambua magari, makasha na dereva
bila kusimamia