Meneja
wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (kushoto) akizungumza
na wanahabari (hawapo pichani) , anayefuata ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja
wa TTCL, Laibu Leonard.
Meneja
wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (katikati) akizungumza
na wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa
TTCL, Laibu Leonard na Kushoto ni Ofisa habari wa TTCL.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam juu ya huduma hiyo, Meneja Huduma za Intaneti
wa TTCL, Abdul Mombokaleo amesema kampuni ya Simu Tanzania imeamua
kuzindua promosheni mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa fursa ya mteja wa
TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia
modem.
"...TTCL
siku ya leo imezindua promosheni mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa
fursa ya mteja wa TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi
na kujipatia modem ya bure.
Akifafanua
zaidi Mambokaleo alisema promosheni hiyo mpya ya “Dili la Ukweli”
inatoa fursa kwa wateja kufurahi modem ya bure pamoja na vifurushi
ambavyo vimepunguzwa bei kwa kiwango ambacho Mtanzania wa kawaida
anaweza kuimudu.
Aidha
akifafanua juu ya utaratibu wa promosheni alisema ili mteja apate modem
ya bure Mteja atapaswa kununua intaneti bila kikomo kwa shilingi
20,000/- tu ambayo itatumika ndani ya mwezi mzima na huduma hiyo ni kwa
wateja wapya tu.
"...Kwa
mteja wenye modem tumewapa fursa ya kuchagua vifurushi ambavyo
vimepunguzwa bei. DILI LA UKWELI inatoa fursa kwa wateja kufurahia
punguzo la bei ya vifurushi vya intaneti vya siku, wiki na mwezi kwa bei
nafuu sana. Intaneti ya TTCL inaubora, ina kasi na uwakika, kwani
teknolojia inayotumika ni ya kuaminika zaidi. Katika kuhakikisha wateja
wa huduma ya intaneti wanafurahia zaidi, TTCL imeshusha bei ya intaneti
ili kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wake.