Makundi ya mashabiki mitandaoni maarufu kama TEAMS yamekuwa ni sehemu
ya maisha ya mtandaoni ya wasanii na watu maarufu wengi hapa nchini.
Linapokuja swala ya ushabiki na mada nzito team hizi huvutana kwa
kutupiana maneno na wakati mwingine hadi maneno makali.
Siku za hivi karibuni baada ya mwigizaji Wema Sepetu alipoachana na
mpenzi wake Diamond Platnum, na badaye Diamond kuamua kutoka na
mwanamama Zari kutoka nchini Uganda, Mashabiki (TEAM) wa Diamond na wale
wanaomponda Wema Sepetu wamekuwa kwakiasi kikubwa
wakiwatupia maneno na
vijembe wale mashabiki wa Wema (TEAM WEMA), kwa picha na maneno.kiasi
ambacho TEAM WEMA kuonekana kama” LOSSERS”.
Lakini leo hii upepo umebadilika huko mitandaoni na TEAM WEMA
wanaonekana kuwa na nguvu zaidi, baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuachia
baadhi ya picha akiwa nchini Ghana akifanya kazi na Van vicker ambae ni
msanii mkubwa hapa Afrika.
Team Wema wamepongeza sana juhudi za mwigizaji huyo kutaka kuivusha
tasnia ya filamu hapa nchini na kuipeleka kimataifa hivyo wanataka Le
Projectii iemdelee
Bongomovies pia inampongeza na kunampa moyo katika juhudi zake hizi
za kukuza tasnia yetu.Hiyo ni moja ya picha za project hiyo mpya
BONGO MOVIES