Akizungumza
jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka
nchini TFF, Boniface Wambura amesema waliopata Beji hizo ni pamoja na
mwamuzi mwanamke aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe, Jonesia
Rukyaa.
Wanawake wengine ni Florentina Zablon toka Dodoma na Sophia Ismail toka Mara kama waamuzi wa kati huku waamuzi wasaidizi wakiwa ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary toka Tanga, Grace Wamala toka Kagera na Dalila Jaffary toka Zanzibar.
Wambura aliwataja wengine kuwa ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin Saanya wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama waamuzi wa kati huku Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Frednand Chacha wa Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.
Wambura amesema, Tanzania imepata beji nyingi za FIFA kwa upande wanawake msimu huu wa 2015 kwani haijawahi kupata beji zaidi ya nne kuanzia ianze kutoa waamuzi wa kike kwani hata mwaka huu haikuwa na mwamuzi mwenye beji wa kike.
Waamuzi wa kike ambao walishawahi kuwa na beji za FIFA kuanzia 2006 ni Flora Kashaija, Isabela Kapera na Judy Gamba kama waamuzi wa kati na waamuzi wasaidizi ni Zahara Mohamed, Saada Tibabimale, Mwahija Omary toka Zanzibar.

EATV.TV