Dec 23, 2014

POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA MACHINGA WALIOANDAMANA JIJINI DAR LEO

 Wanausalama wakiwa eneo la tukio.

 Moto uliowashwa na machinga ukiwaka barabarani eneo la Kamata, Kariakoo jijini Dar leo.
 Gari la zimamoto likiwasili eneo la kamata kuzima moto uliowashwa na machinga.


 Mawe yaliyowekwa barabarani na machinga wakati wakiandamana kuelekea ofisi za jiji.


 Wananchi wakishirikiana kuondoa mawe barabarani ili kuruhusu magari kuendelea na safari zake.
ESHI la Polisi jijini Dar limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la Machinga waliokuwa wanaandamana kuelekea ofisi za jiji eneo la Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Machinga hao waliamua kuchoma matairi na kuweka mawe barabarani wakati wa maandamano hayo ambapo madai yao ni kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa na askari wa jiji ikiwemo kunyang'anywa mali zao.
(PICHA NA MAKONGORO OGING' / GPL)