Mbunge wa chama tawala cha
Conservative nchini Uingereza , amekiri kucheza mchezo maarufu kwenye
tabiti yake wakati wa kikao cha kamati moja la bunge hilo.
Jarida
la The Sun, limechapisha picha za mbunge huyo kwa jina Nigel Mills
akicheza Candy Crush Saga kwenye tabiti yake, wakati wa mkutano wa
kamati hio kuhusu mageuzi ya sera ya serikali kuhusu malipo ya uzeeni.Jarida hilo linasema Bwana Nigel alicheza mchezo huo kwa zaidi ya saa mbili.
Hata hivyo amejitetea akisema alifahamu kilichokuwa kinaendelea katika kamati hiyo na kwamba lihusika katika kuuliza maswali. Hata hivyo alikiri kucheza mara mbili na kusema atajaribu kujizuia kucheza mchezo huo katika siku za usoni akiwa kazini.
