undi kongwe la sanaa ya uigizaji na ngoma lililotoa vipaji vingi vya
uigizaji hapa nchini, Kundi la Sanaa la Kaole “Kaole Sanaa Group”
limerudi ila sasa kwa jina lingine..habari kamili ametueleza hapa,
Halima Yahya “DAVINA”moja kati ya waliokuwa kaole na sasa wameasisi hii
kaone, anasema;
"Wapenzi wetu wa tamthilia na filamu za kibongo...mimi km
mimi nimekua nikipokea maoni ya watu wengi hapa na hata mikoani kwamba
wamemiss tamthilia zetu za zamani zilizokua zimejaa maadili na
mafundisho nami kwa kushirikiana na wenzangu kadhaa tuliokua ktk kundi
la maigizo la KAOLESANAAGROUP tumeamua kulirudisha kundi ila kwa sasa litaitwa KAONE
na tutakuemo wasanii wengi wa zamani kidogo akiwepo Nyamayao, kibakuri,
Muhogo Mchungu, bi Star, Thea,Coletha,Ndumbagwe na wasanii kibao
uwajuao."
Pia akaeleza siku ya uzinduzi rasmi wa kundi hilo;
“Tutalizindua rasmi kundi letu cku ya tar 26 meezi huu wa 12 pale Darlive Mbagala mtapata kuona mengi tuliyowaandalia pia na tamthilia yetu mpya iitwayo KIPUSA itakayoanza kuruka hewani tarehe 5 mwezi wa kwanza katika kituo cha televisheni cha Tv1.
Karibuni sana sana na tunawaahidi vitu adimu mlivyovikosa muda mrefu....tunawapenda san bila nyinyi hakuna sisi"....Davina alimaliza.
Pichani ni baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo, wakiwemo, Davina, Nyamayao nawengineo.Ngoja tusubiri tuone moto wao....