kimasai nchini kenya.Aliposafiri
nchini Kenya mwaka 2011 kama mtu aliyejitolea katika shirika moja lisilo
la kiserikali ,uamuzi wa kuwa kijana wa kimasai wa Ilchamus lilikuwa
wazo la mwisho katika akili ya Max Roing,ambaye ni raia wa Sweden.Lakini
miaka mitatu baadaye ,Max mwenye umri wa miaka 25 amependa sana
utamaduni wa watu hao walio wachache katika fukwe za ziwa Baringo.
Max
pia alikuwa miongoni mwa vijana 5,000 wa Ilchamus katika kaunti ya
Baringo waliotawazwa kuwa wanaume kamili baada ya kupashwa tohara.
''Nilikuja nchini Kenya kama mtalii na pia kusaidia kuhifadhi
mazingira kupitia upandaji wa miti katika kaunti ya kajiado''bwana Roing
aliliambia gazeti la Nation nchini Kenya baada ya kuhitimu.
Kwa
sasa anafuata mila yake mpya inayoshirikisha mavazi yanayovaliwa pamoja
na shuka nyeusi,simi iliofungwa katika ukanda wake wa rangi ya
hudhurungi,viatu vyeusi na nguo iliorembeshwa kwa shanga.
Hafla hiyo ya kuhitimu imemfanya kuingia katika umri wa Ilmeng'ati.
''Mimi
ni Max Lemeyan Le Kachuma kutoka kabila la Ilchamus na ukoo unaojiita
Iltoimai''alisema jina lake huku akinywa maziwa yalio chungu katika
kikombe.