.jpg)
Mwanamuziki
nguri wa muziki wa dansi nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na
karibuni amezindua sinema iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika jamii.
Katika
filamu hiyo ambayo Kitime anacheza kama muigizaji mkuu, akitumia jina
la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye nyumbani kwake kuna umemejua
akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na baadhi ya wakazi wenzake
kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani kwake.
Kwa
kutumia ofisi yake, anapora ardhi za watu na mbaya zaidi anawachukia
wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi anaona hawana lolote zaidi ya
kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano na migogoro mikubwa
ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na msisimko wa
namna yake.
Filamu
hiyo ambayo imeandikwa na Irene Sanga chini ya utayarishaji wa Sylone
Malalo na kuongozwa na Simon Mwakifwamba, msambazaji mkuu ikiwa kampuni
ya Proin Promotion, licha ya pia ina muigizaji mahiri nchini, Charles
Magari ‘Mzee Magari’.
Mtayarishaji
wa filamu hiyo, Malalo anasema movie hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko
makubwa katika tasnia ya filamu nchini na anawataka wale ambao
wanapenda vitu tofauti kuangalia pia inashirikisha wasanii wa Sanaa za
mapigano ‘martial arts’.
Magari
ambaye anaigiza kama mtu ambaye anataka mabadiliko kijijini hapo na
kuondokana na urasimu na ukiritimba wa Mzee Nongwa, ina waigizaji mahiri
ambao pia ni walimu wa Sanaa katika Taasisi ya Sanaa (Tasuba) ambao ni
na Thabit Hudu na Mwanaidi Zambo.
Filamu
hiyo ni kazi ya kwanza pia ya mzalishaji Malalo ambaye amebobea katika
utengenezaji wa picha za video, documentary na filamu mbalimbali za
kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa ni
katika jamii na baadhi ya filamu hizo ni pamoja na ‘Zawadi’ na zingine.
KWA HISANI YA BONGO MOVIE & JIACHIE BLOG
.jpg)
.jpg)
.jpg)