Leo mwanadada Zamaradi mketema ameamua kusema haya kuhusu filamu
zetu nchini. Kama wewe ni mdau wa bongo movies tafadhali tusaidie kutoa
maoni yako juu ya maswali haya ambayo zamaradi anauliza…
Hichi ndicho alichosema…
“…Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu... R.I.P KANUMBA
alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu
aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!
Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..?
Kwanini wasanii wetu
wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!?
Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana
kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya
vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa
tunapwaya kiasi gani.. Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza
utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na
nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni
kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana.. nahisi sasahivi tunafanya
filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi
tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika
sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi
uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo
inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!!
kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??
Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye
tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa
tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni
juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee
wapenzi.. mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPIII…!!???