Dec 7, 2014

Alichokisema JB kuhusu soka la bongo. Asikitishwa na uchovu wa wachezaji.

Alichokisema JB kuhusu soka la bongo. Asikitishwa na uchovu wa wachezaji.
Kupitia mtandao mmoja wa kijamii nchini, mwigizaji nguli Jacob Steven – JB ameamua kufunguka haya yake ya moyoni kuhusu mpira wa kibongobongo
“Wapenda kandanda kama mimi hembu tujadili kidogo nyinyi mnaonaje? hivi mbona mimi sielewi? ni kweli hata mimi nafurahia ujio wa
wachezaji wa kigeni kwamba wataleta changamoto lakini hawa wa kwetu wamekumbwa na nini? mbona mchezaji anacheza msimu mmoja tu kwisha? leo hii angalia timu ya taifa ukiacha kina Samatta hatuna mshambuliaji, hamuoni wivu wachezaji wa nje wanakuja kuzoa milion na kuondoka?
Amkeni tutapata  wachezaji watakao cheza kwa muda mrefu kama rafiki yangu Madaraka Suleiman.
Jana nilikuwa naongea na kocha wa Exp.ya Uganda juu ya wachezaji wao walio hapa, anatamba bado wana wachezaji wengi vijana ambao ni wazuri sana.”
We una maoni gani kuhusu soka letu hili?