
Kamishna
wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine
kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
(TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi
wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji
Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji
Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.
Kamishna
Msaidizi Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje,
akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria
mkutano huo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick
Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo.
Kamishna
wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) katika picha ya
pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba ambao
umewajumuisha wafanyabiashara wa madini ya Shaba, wachimbaji wadogo,
viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishna Wasaidizi wa Madini
kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini
Wakaazi.
Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam
Wizara
ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya Shaba katika
mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014 na
kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo,
viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini
kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini
Wakaazi.
Akifungua
mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta
ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea thamani madini hayo,
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja amewataka wachimbaji
wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini
ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza shughuli za uchimbaji wa
madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea thamani madini hayo.
Aidha,
Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji na
wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na taratibu
kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia
madini hayo kutokupata thamani halisi.



