
Spika
wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiliongoza Bunge mjini Dodoma leo,wakati
akitoa ufafanuzi kuhusu mtu mmoja kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma kwa kosa la kupatikana akisambaza Ripoti ya (ESCROW) ya Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Sheria Baada ya Hoja
iliyoibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia.

Mbunge
wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia akiwa amekaa na Hasimu wake wa Siasa
jimbo la Vunjo Mhe.Agustino Mrema wakimsikiliza kwa makini Spika wa
Bunge Mhe.Anna Makinda.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana ya wanachama wa chama cha kuweka na
kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda. Aliye valia gauni la njano ni
Mbunge wa Busanda Mhe.Lolesia Bukwimba.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda.

Mbunge
wa Busanda Mhe. Lolesia Bukwimba (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa
nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya juu ya ugeni wake
wa wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka
Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma leo.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka
Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma leo.

Waziri
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sofia Simba (kushoto)
akifurahia jambo na Mhe.Anna Mkinda wakati wakitoka katika kikao cha
Bunge leo. Picha zote na Deusdedit Moshi